Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 13.02.2019:


Zinedine Zidane

Real Madrid wanaamini wakati mgumu anaopitia kocha wa Chelsea Maurizio Sarri utawarahisishia kumsajili kiungo Mbelgiji Eden Hazard, 28, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Chelsea wanata kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya Sarri ambaye amekuwa akisuasua. (Sun)

Simba yawika dhidi ya Al-Ahly ya Misri kombe la Caf

Ramsey asaini makubaliano ya kujiunga na Juventus

Golikipa wa Paris St-Germain Gianluigi Buffon, 41, amesema kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu itakuwa ni namna bora kwake yeye kustaafu kucheza mpiara. (Telegraph)


Gianluigi Buffon

Real Madrid wataminyana Barcelona kumsajili streka wa Benfica Luka Jovic, 21, kwa kutangaza dau la euro milioni 45 kwa nyota huyo anayechezea kwa mkopo klabu ya Eintracht Frankfurt. (Bild - in German)

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 12.02.2019

Wawakilishi wa mchezaji wa Everton raia wa Brazil Richarlison, 21, wamefanya mazungumzo na hav Atletico Madrid kuhusu mshambuliaji huyo kuhamia vigogo hivyo vya Uhispania. (AS - in Spanish)

Kiungo Mjerumani wa Arsenal Mesut Ozil amekuwa akipigiwa chapuo katika vilabu vingine na wawakilishi wake, huku mustakabali wake dimbani Emirates ukibaki kuwa wa mashaka. (Telegraph)


Mesut Ozil

Beki wa kulia wa Crystal Palace Muingereza Aaron Wan-Bissaka anatakia na klabu ya Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye miaka 21 pia anatakiwa na Manchester City. (Sun)

Tottenham inataraji kumsajili winga wa Inter Milan na timu ya taifa ya Croatia Ivan Perisic, 30, ambaye alikuwa aknyemelewa na Arsenal mwezi Januari. (Tuttosport, via Football Italia)


Ivan Perisic

Mchezaji wa zamani wa Manchester United raia wa Ureno Luis Nani, 32, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Sporting CP, ananyemelewa na klabu ya Ligi ya Marekani MLS side Orlando City. (Marca - in Spanish)

Winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, anaongea kwa ishara tu na wachezaji wenzake wa Real Madrid kwa kuwa bado hajajifunza Kihispania, amesema mchezaji mwenzake Marcelo. (Marca)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.