Mhudumu aliyeanguka kutoka kwenye ndege Uganda afariki dunia


Ripoti zinasema mhudumu wa ndege alikuwa akifanya maandalizi kwa ajili ya abiria kuingia

Mfanyakazi wa Ndege aliyeanguka kwenye mlango wa dharura wa ndege kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda ameaga dunia, BBC imeelezwa

Mwanamke huyo ambaye uraia wake haujabainishwa, alikimbizwa Hospitali ya Kisubi umbali wa Kilomita 16 lakini alipoteza maisha baadae,Msemaji wa Shirika la Emirates alieleza.

Ripoti zinasema kuwa tukio la kuanguka lilitokea wakati mhudumu huyo alipokuwa akiandaa ndege kwa ajili ya kupandisha abiria.

Mhudumu aanguka kutoka kwenye ndege Uganda

Tanzania kati ya nchi raia hawana furaha duniani

Mamlaka ya anga nchini Uganda imesema inafanya uchunguzi.

Imesema katika taarifa yake kuwa mhudumu huyo ''alikuwa amefungua mlango wa dharura'' na ''bahati mbaya'' alianguka nje ya ndege hiyo iliyokuwa imepaki baada ya kutua

Msemaji wa hospitali ya Kisubi, Edward Zabonna ameiambia BBC kuwa mfanyakazi huyo alikuwa na majeraha ''usoni mwake na miguuni''

Alisema alikuwa'' amepoteza fahamu lakini alikuwa hai'' alipowasili hospitalini, siku ya Jumatano jioni lakini alifariki muda mfupi baadae.

Shirika la Habari la Ufaransa limenukuu taarifa ya Emirates ikisema ''Mfanyakazi wetu bahati mbaya alianguka kutoka kwenye mlango uliokuwa wazi wakati akiandaa ndege kwa ajili ya abiria kuingia.
Shirika hilo limesema litatoa ushirikiano kwa uchunguzi utakaofanyika.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.