mwanaharakati aliyepotea kenya apatikana amefariki


Mwili wa mwanaharakati nchini Kenya Caroline Mwatha umepatikana, msemaji wa polisi Charles Owino ameithibitishia BBC.

Duru zinaarifu kwamba mwili wa marehemu umepatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City Mortuary mjini Nairobi.

Caroline Mwatha ni mwanaharakati aliyefanya kazi katika shirika la haki la kijamii katika kitongoji cha Dandora mjini Nairobi, shirika linalonakili visa vya mauaji ya kiholela yaliotekelezwa na maafisa wa polisi hususan katika vitongoji vinavyoshuhudia uhalifu mkubwa Nairobi.

Washukiwa wa mauaji ya watoto Tanzania wapandishwa mahakamani

Muhandisi maarufu wa Tanzania ashinda tuzo Marekani

Wizi wa mti ulio na miaka 400 wazua majonzi Japan

Caroline inaarifiwa ni mke na mama wa watoto wawili na anatambulika pakubwa kwa mchango wake katika jamii.

Alionekana mwisho Jumatano wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Kenya, Caroline amekuwa akinakili visa vya mauaji yaliotekelezwa na maafisa wa polisi Kenya na visa vya watu kutoweka kiholela.

Baada ya jitihada za wiki nzima, leo uthibitisho umetoka kwamba amefariki.

Duru zinaeleza kwamba alifikishwa katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti na mtu binafsi - haijulikani wazi ni lini hasaa alipopelekwa.

Polisi sasa inajaribu kuchambua ni wapi na vipi alipofariki.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.